Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome,Int.34P, Via Gorgona 48, 00139 Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---
TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Wednesday, May 16, 2012

BREAKING NEWS: TAARIFA ZA MSIBA MJINI ROMA

UJUMBE KUTOKA KWA KATIBU WA CHAMA CHA WANAFUNZI WATANZANIA WAKATOLIKI ROMA
WAPENDWA WANA UMOJA, TUMSIFU YESU KRISTU!
KWA NIABA YA MWENYEKITI WETU PADRI RICHARD TIGANYA, NA UONGOZI MZIMA TUNAPENDA KUWAPA TAARIFA ZA KIFO CHA GHAFLA CHA MHESHIMIWA PADRE JAMES AMON MBWANA WA JIMBO KATOLIKI LA MBEYA KILICHOTOKEA LEO HAPA ROMA.
MAREHEMU PADRE JAMES ALIKUTWA NA MAUTI ALIPODONDOKA GHAFLA MAENEO YA TERMINI AKIWA NJIANI KWENDA CHUO.
MPENDWA PADRE JAMES ALIKUWA ANAISHI ZAGALORO NA ALIKUWA ANASOMA LUGHA YA KILATINI NA KIGIRIKI CHUO CHA MTAKATIFU AUGUSTINO.
KWA SASA MWILI WA PADRE JAMES UKO KATIKA CHUMBA CHA MAITI NA MAENEO YA TERMINI NA TARATIBU ZINGINE ZINAFANYIKA.
TUNAWAAHIDI KUWAPA TAARIFA ZAIDI ZA NINI KITAFATA HASA SWALA LA KUMUAGA.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA.......!
PADRE CHRISTIAN LIKOKO
KATIBU

JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA IMESIKITISHWA SANA NA KIFO HICHI CHA GAFLA CHA PADRE AMON MBWANA. TUNAWAPA POLE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU. MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAREHEMU PADRI JAMES AMON MBWANA MAHALI PEMA PEPONI AMINA.

More Pictures of Tanzania Muungano Day in Rome










Monday, May 14, 2012

More Photos of the Tanzanian Union Day in Rome


Wakina mama wakisikiliza kwa umakini speech toka kwa mh. Balozi.  
Esther Raphaely akingia ukumbini.

    Picha ya pamoja na Balozi.
Flowers zilipendezesha Sherehe hii.
Wakina mama walipendeza kuliko.
 Watanzania wakiimbaa wimbo wa Taifa
 Watanzania wakiimba wimbo wa Taifa
Baada ya Wimbo wa Taifa

Sherehe ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Roma yafana.



Kwa mbali Mama Tandika pamoja na Mama Mhella nao walikuwepo.



     Dj. Beka alizungukwa na mashine ya nguvu.

Ile sherehe ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa na wengi mjini Roma, ilifanyika jumamosi tarehe 12 Mei 2012.Sherehe ilifanyika kwenye ukumbi wa Karispera club 69, uliopo katikati ya mji mkuu Roma na kuudhuliwa na Watanzania wengi kutoka sehemu mbalimbali za Italia. Mgeni rasmi alikuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela, ambaye kwa mara ya kwanza alikutana na Watanzania kwa pamoja kutoka kila kona ya Italia. Kwenye sherehe hii, balozi Msekela aliishukuru Jumuiya ya Watanzania Roma kwa kuandaa sherehe hii muhimu kwa Taifa la Tanzania kutokana na dhumuni lake la kusherekea muungano ambao ni moja ya ngao ambazo tuliachiwa kama urithi na baba wataifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume. Balozi Msekela pia aliwaelezea Watanzania kuwa amefurahishwa sana na umoja ambao ameuona kwenye siku chache toka kufika kwake nchini Italia na kuwaomba Watanzania waendelee na moyo huu wa ushirikiano maana ndio kitambulisho cha Tanzania nje ya nchi. Balozi alihaidi kushirikiana na hizi jumuiya za Kitanzania hapa Italy na kuwaomba wasisite kwenda kumuona pale watakapo kuwa wanaitaji ushauri na msaada wa aina yeyote toka ofisini kwake.

Mungu Ibariki Tanzania
( Picha na George Mayaka) zingine zitafuata muda si mrefu.


Friday, May 11, 2012

Balozi Dr.James Msekela kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Muungano

Ile siku ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania iliyokuwa inasubiliwa na Watanzania wengi Italia ndio hiyo imewadia. Mgeni rasmi kwenye sherehe ya kesho (12.05.2011) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. Dr. James Msekela. Watanzania mnaombwa mfike kwa wingi ili tushereke kwa pamoja kwa style yake sikukuu hii muhimu kwa taifa letu. Anwani ya sehemu ni Via Angelo Emo 69, katikati ya mtaa unaokutanisha Metro Cipro na Metro Valle Aurelia. Kwa yoyote atakayepotea anaweza kumpigia Katibu kwa namba hii 3479094800. Sherehe itaanza saa kumi na moja jioni mpaka Lyamba,Kutakuwa na nyama choma, chakula cha Tanzania, vinjwaji na mengineyo..

Tuesday, May 8, 2012

Mkapa amkaanga Live Mh. Raisi Juu ya Mjengo wa Ubalozi Mjini Rome


RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, jana aliikaanga serikali ya Jakaya Kikwete mahakamani akidai kuwa hakuna ubadhirifu wowote uliofanywa na aliyekuwa Balozi wa Italia, Prof. Costa Mahalu, katika ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo.
Akiongozwa na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, baada ya kuapa alieleza kuwa kati ya mwaka 1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya Kikwete alikubaliana na ununuzi huo.
Mkapa ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa, Profesa Mahalu akiwa balozi.
“Serikali yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu,” alidai Rais Mkapa.
Mahalu anatuhumiwa kuidhinisha kwa niaba ya serikali ununua wa jengo la ubalozi kwa thamani ya euro milioni 3 kwa njia ya mikataba miwili na kwa akaunti mbili.
Mawakili: Wewe au serikali ya awamu ya tatu iliwahi kupokea malalamiko toka serikali ya Italia kuwa ubalozi wetu nchini humo ulivunja sheria kuhusu mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Hapana, sijawahi kupokea malalamiko.
Mawakili: Ukiwa Rais hujawahi kupokea malalamiko kuwa fedha za serikali yetu zilizotumwa kwa ajili ya kumlipa muuzaji wa jengo hilo kuwa hazijamfikia?
Mkapa: Hadi leo hii natoa ushahidi hapa mahakamani sijawahi kupokea malalamiko ya aina hiyo.
Mawakili: Uliwahi kupata malalamiko toka kwa CAG, Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wala Ofisi ya DPP kuhusu ubadhirifu wa ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Sijawahi kupata.
Mawakili: Nini ufahamu wako kuhusu utumishi wa Profesa Mahalu?
Mkapa: Namfahamu kama msomi mzuri, mchapakazi, muadilifu na kiongozi anayetenda haki.
Mawakili: Mawasiliano kati ya serikali na balozi yanafanyika kwa njia zipi?
Mkapa: Balozi anaweza kuwasiliana na serikali yake kwa njia ya barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Rais au kwa njia ya mdomo. Na mawasiliano siyo lazima yafanyike kwa njia ya maandishi tu kwa sababu maelekezo mengine ambayo anapewa balozi na serikali yake ni ya siri kwa maslahi ya taifa hivyo anaweza kuitwa nyumbani na kupatiwa maagizo hayo kwa njia ya mdomo.
Mawakili: Kwa wadhifa wako ule wa urais, kabla ya kwenda kuzindua jengo hilo Januari 23, 2003, hukuwahi kupokea taarifa toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP za kukukataza usiende kuzindua jengo hilo kwa sababu kulikuwa na harufu za ubadhirifu wa fedha za umma?
Mkapa: Ofisi hizo hazikuwahi kunipatia taarifa hizo.
Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili wa serikali
Mawakili: Hebu ieleze mahakama ni kwa nini bei za jengo zinatofautiana maana risiti za manunuzi zinaonyesha lilinuliwa kwa euro milioni 3 na hansard ya Bunge iliyosomwa na Kikwete bungeni mwaka 2004 inasema ilinuliwa kwa shilingi bilioni 2.9?
Mkapa: Kazi yangu siyo kufanya uthamini wa fedha za kigeni kwamba wakati huo hizo euro milioni 3 zilikuwa na thamani gani kwa fedha Tanzania (kicheka).
Mawakili: Nani aliagiza upelelezi wa manunuzi ya jengo la Italia ufanyike?
Mkapa: Sijui.
Mawakili: Uchunguzi wa jengo hilo ulifanyika wakati wewe ukiwa madarakani?
Mkapa: Sijui, nilikuja kuona Balozi Mahalu kashtakiwa mwaka 2007 nikiwa tayari nimestaafu. Nilithibitisha taarifa hizo kupitia vyombo vya habari kuwa ameshtakiwa.
Mawakili: Nani alikupa taarifa za muuzaji wa jengo hilo anataka kulipwa kwa mtindo huo wa akaunti mbili?
Mkapa: Ni Mahalu na alinipa taarifa kwa mdomo na alikuwa ameandaa ripoti juu ya ununuzi na akawa anaomba ridhaa ya serikali kabla ya kulinunua.
Mawakili: Ulisema hukuweza kuzuia ununuzi wa jengo, je ulikuwa na madaraka ya kuweza kuzuia lisinunuliwe?
Mkapa: Eh! Mimi ndiye nilikuwa Rais wa nchi; nilikuwa na madaraka hayo na badala yake fedha hizo zingeelekezwa kwenye mahitaji mengine ila kwa sababu nilikuwa ninajua umuhimu na faida ya nchi kununua jengo lile ndiyo maana nikaridhia kwa mdomo linunuliwe.
Wakili: Ulitoa maelekezo kwa nani?
Mkapa: Nilitoa maelekezo kwa njia ya mdomo kwa watendaji na maagizo hayo yalipaswa yatekelezwe na Wizara ya Mambo ya Nje na ilikuwa jukumu la Mahalu kuieleza wizara hiyo na ubalozi utekeleze maagizo yangu.
Wakili: Kwa hiyo unaieleza mahakama kuwa Wizara ya Mambo ya Nje, ilituma malipo kwa mtindo wa akaunti mbili tofauti?
Mkapa: Inahusu nini sasa? Mimi nilitoa maagizo, hivyo lilikuwa ni jukumu la Balozi Mahalu kuieleza wizara yake. Sasa suala la hayo makaratasi ya kufanya mchakato wa kulinunua, mimi kama Rais siwezi kuingilia. Watendaji walipaswa watekeleze.
Mawakili: Utajisikiaje tukikwambia kuwa yule muuzaji aliyetuuzia jengo kwa mtindo wa akaunti mbili alikuwa akikwepa kodi kwa serikali ya Italia?
Mkapa: Aaah! Mi’ sioni tatizo; kikubwa hapa Tanzania tumepata jengo, Alhamdulilah (kicheko).
Mawakili: Utajisikiaje ukisikia Mahalu alitumia zile euro milioni 3 kwa matumizi yake binafsi?
Mkapa: Nitashangaa sana. Pia wewe wakili wa serikali ndiyo nitakushangaa zaidi kwani hansard ya Bunge iliyosomwa na Kikwete bungeni imetamka bayana kuwa serikali ilimlipa muuzaji wa jengo na kwamba taratibu na sheria ya manunuzi ya umma zilifuatwa na hadi sasa huyo muuzaji hajawahi kulalamika kuwa hajalipwa fedha zake.
Rais Mkapa aliingia mahakamani hapo saa 3:45 asubuhi akiwa katika gari aina VX lenye namba T 745 BQE akiongozwa na walinzi wake.
Maafisa toka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) walionekana kuingia katika viwanja vya mahakama hiyo kabla ya kiongozi huyo kuwasili.
Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta, aliahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo mshtakiwa wa pili aliyekuwa Meneja Utumishi na Utawala wa Ubalozi huo, Grace ataanza kujitetea
Source: Maggid Mjegwa Blog

Sherehe ya Muungano wa Tanzania Jumamos hii 12 Mei 2012


Jumuiya ya Watanzania Rome, inapenda kuwakaribisheni Watanzania wote nchini Italy kwenye sherehe ya Muungano wa Tanzania. Sherehe Itafanyika jumamos ya wiki hii tarehe 12 Mei 2012, kwenye Ukumbi wa Karispera Club 69, uliopo kwenye Mtaa wa Via Angelo Emo 69 mjini Rome, kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka Lyamba! Kwa wale wote watakaotaka kushiriki mnaombwa muandike e-mail (watanzaniaroma.yahoo.it) au mpige simu 3479094800 ili muweze kupata maelezo zaidi ya namna ya kushiriki. Ticket zipo tayari na unaweza kuzipata kwa kumcontact Mwenyekiti, Mh. Leonce Uwandameno au Katibu (Nd. Andrew Chole Mhella) kwa contact za hapo juu.Tafadhali kwa wale wote watakao kuja mnaombwa msisahau ticket zenu.Kwa wale ambao watashindwa kupata ticket kabla ya siku ya sherehe mnaweza pia kuzipata mlangoni kwenye ukumbi.
NB: Itakumbukwa kuwa sherehe hii ilipaswa kufanyika tarehe 28 Aprili 2012, lakini kwa kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu tukaisogeza mbele wiki mbili.
Asanteni na Karibuni sana
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Jumuiya ya Watanzania Roma.
Katibu,
Andrew Chole Mhella.